Moja kati ya makinda wengi waliofika Chelsea na kulelewa hapo ata kabla ya kutimiza miaka nane, Harvey St. Clair amemaliza mkataba wake na Chelsea na mpaka sasa hajasaini mkataba mpya wa kusalia klabuni hapo kwa kipindi kingine.
Kutokusaini kwake mkataba kunamfanya kuwa huru kusaini na kujiumga kwenye klabu yoyote na sasa anatajwa kufukuziwa na klabu ya Venezzia.
Klabu hiyo ya Venezzia inayofundishwa na gwiji Pipo Inzaghi inashiriki ligi daraja la kwanza nchini Italia maarufu kama Serie B inatajwa kumfukuzia nyota huyo mwenye miaka 19 kwa sasa na ipo karibu kumnasa.
No comments:
Post a Comment