Rasmi; Chelsea yakamilisha mpango wake wa kuvuna pesa kibao - Darajani 1905

Rasmi; Chelsea yakamilisha mpango wake wa kuvuna pesa kibao

Share This

Acha nianze kwa kutoa shukrani kwa Mwenyezi Mungu kwa kunipigania afya na uzima wangu mpaka leo nazidi kukuletea habari na tetesi kibao kuhusu klabu yetu pendwa, klabu ya Chelsea. Ndani ya siku mbili tatu hizi nimesumbuliwa na magonjwa lakini Mungu ni mwema naendelea kuimarika na kuwa sawa kila sekunde na dakika zinavyozidi kusonga.

Sasa turudi huku kwenye habari. Nadhani unakumbuka niliwai kukuletea habari ambayo ilikaa kimtindo wa fununu kuhusu Chelsea kukaribia kuupata udhamini na kampuni ya utengenezaji na uuzaji wa magari ya Hyundai? nikakudadavulia kwa undani kwamba Chelsea itakuwa klabu inayovuta fungu kubwa la pesa kutokana na udhamini huo? Na nadhani unatambua kwamba lile tangazo la 'Alliance' kwenye mkono wa kushoto wa jezi za Chelsea ilikuwa ni nyongeza waliyopewa kampuni ya Yokohama ambao ni wadhamini wakuu watangaze kwa msimu mmoja bila malipo, kwa hiyo lile tangazo la Alliance lilikuwa linamilikiwa na kampuni ya Yokohama.

Sasa ipo hivi mara baada ya msimu mmoja wa tangazo hilo la nyongeza kuisha sasa Chelsea imeingia rasmi mkataba mpya na mdhamini huyu wa Hyundai ambaye yeye tangazo lake litakuwepo upande uliokuwa unakaa tangazo 'Alliance' yaani mkono wa kushoto wa jezi za Chelsea kwa miaka minne yaani mpaka mwaka 2022 kwa timu zote yaani Chelsea FC ambayo tunaijua wengi, Chelsea FC Women hii ni kwa ajili ya soka la wanawake pamoja na klabu zote za vijana wa akademi ya Chelsea.

23-Julai-2018 ndiyo itakuwa siku ya kwanza kwa Chelsea kuvaa jezi ikiwa na tangazo la kampuni hiyo pale itakaposafiri mpaka nchini Australia kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Perth Glory.

Sasa ukitaka kujua kuhusu ni kiasi gani Chelsea itavuna kwenye biashara hii na habari nyengine zote kuhusu biashara hii, bonyeza hapa

No comments:

Post a Comment