Mshambuliaji wa Chelsea, Olivier Giroud juzi alipata majeraha wakati akiitumikia timu yake ya taifa ya Ufaransa ilipokuwa ikicheza mchezo wake wa kirafiki wa kujiandaa na michuano ya kombe la dunia itakayoanza siku kadhaa zijazo huko nchini Urusi.
Kwenye mchezo huo wa kirafiki dhidi ya Marekani mshambuliaji huyo mwenye miaka 31 aligongana na mlinzi wa Chelsea, Matt Miazga ambaye ni raia wa Marekani na kusababisha wote kupata majeraha na kuvuja damu lakini hofu kubwa ikibaki kwa Giroud kama je atakuwa sawa kushiriki kombe la dunia lakini haswa kuwepo kwenye kikosi kitakachocheza mchezo wa kwanza wa michuano hiyo dhidi ya Australia?
Hatimaye kocha wa timu hiyo ya taifa la Ufaransa, Didier Deschamps alifanyiwa mahojiano na kuthibitisha majeraha aliyoyapata nyota huyo ni madogo na atakuwepo kwenye kikosi kitakachocheza mchezo wake wa kwanza wa kombe la dunia dhidi ya Australia.
No comments:
Post a Comment