Siku na saa zinazidi kuyoyoma kabla ya michuano ya kombe la dunia kuanza huko nchini Urusi. Leo zimesalia siku 4, kesho zitakuwa zimesalia siku tatu. Siku zinazidi kwenda na hakika kuna siku itafikia zitakuwa zimesalia dakika kadhaa tu kabla ya mwamuzi kupuliza kipyenga kwa mara ya kwanza ikimaanisha michuano hiyo ni rasmi imefunguliwa huko nchini Urusi.
Kuelekea kwenye michuano hiyo hapa nitakuwa nakujuza kuhusu michezo ambayo wachezaji wa Chelsea watakuwa wamehusika kwenye michezo hiyo ya kitaifa.
Lakini kabla ya kukuletea habari hizo, hapa nakujuza hali na nafasi ya nyota wa Chelsea katika vikosi vya timu zao za taifa ambazo zitashiriki michuano hiyo.
Ubelgiji
Kuna timu mbili zina wachezaji wengi kutoka Chelsea kwenye vikosi vyao timu za taifa ambazo ni Ubelgiji pamoja na Nigeria. Zote zinawachezaji watatu kutoka klabuni Chelsea, Eden Hazard, Michy Batshuayi pamoja na mlinda mlango Thibaut Courtois. Hazard ana nafasi kubwa kwenye kikosi hiki haswa akitazamwa kama mchezaji nyota wa kikosi hicho wakati kwa upande wa Batshuayi haonekani akitumika sana kama chaguo la kwanza kwa kocha Javi Martinez pamoja na msaidizi wake ambapo kwa nafasi yake kunaonekana kuna upinzani mkubwa kutoka kwa Romelu Lukaku ambaye mara nyingi amekuwa akitumika kama mshambuliaji chaguo la kwanza. Thibaut Courtois hana tabu wala tatizo kwenye nafasi yake ya ulinda mlang akitumika kama chaguo la kwanza.

Ufaransa
Mchezaji bora klabuni Chelsea kwa msimu wa 2017-2018 lakini pia akichaguliwa kuwa mshindi wa tunzo inayotolewa na mdhamini mkuu klabuni Chelsea maarufu kama Yokohama, N'Golo Kante akiwa pamoja na nyota mwengine wa Chelsea, Olivier Giroud wataiongoza vyema timu yao ya taifa katika michuano hiyo huku Kante akiwa hana wasiwasi kwenye nafasi yake ya kiungo ambapo amekuwa akitumika kama mchezaji chaguo la kwanza kwenye kikosi cha kocha Didier Deschamps. Kwa upande wa Giroud ana nafasi kubwa ya kutumika kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo na kama unakumbukumbu vyema nyota huyo usajili wake wa kutua Chelsea akitokea Arsenal ulishinikizwa kwa kiasi kikubwa na kocha huyo ambaye alimwambia nyota huyo mwenye miaka 31 kwamba atafute klabu nyengine na aondoke Arsenal. Anapendwa na kocha huyo na anaweza akatumika kama chaguo la kwanza.

Uingereza
Kiungo wa Chelsea aliyeutumia msimu uliopita kwa mkopo klabuni Crystal Palace, Ruben Loftus-Cheek amepata nafasi kwenye timu hiyo ya taifa na haionekani akiwa na nafasi kubwa ya kutumika kwenye kikosi hicho ingawa anaweza akafanya makubwa kutokana na kocha kumuamini na kuamini kwamba anaweza kufanya makubwa. Gary Cahill, mlinzi na nahodha wa kikosi cha Chelsea amerudishwa tena kwenye kikosi hicho mara baada ya kuachwa kwenye michezo ya kirafiki iliyochezwa mwezi Marchi, lakini nini kimemfanya kurejeshwa? uwezo mkubwa aliouonyesha kwenye michezo ya mwisho ya Chelsea huku akitumika zaidi kama mlinzi wa kati tofauti na hapo kabla alipokuwa akitumika kama mlinzi wa kati ila anayecheza pembeni sana kwenye mfumo wa walinzi watatu kumemfanya kocha wa timu hiyo ya taifa kuweza kumrejesha kikosini. Ana nafasi kubwa kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo ya taifa.

Brazil
Huku kuna mchezaji mmoja tu wa Chelsea, Willian Borges da Silva huku nyota mwenzake wa Chelsea, David Luiz hakufanikiwa kuitwa kwenye kikosi kitakachoshiriki michuano ya kombe la dunia. Willian ana nafasi kubwa kutumika kama chaguo la kwanza kwenye kikosi kilichochini ya kocha Tite. Anaweza akawa mmoja katika safu ya ushambuliaji ya Brazil ambapo inadhaniwa atatumika yeye akiwa sambamba na Neymar pamoja na Gabriel Jesus au Firmino.

Hispania
Nahodha msaidizi wa Chelsea, Cesar Azpilicueta Tanco ni mchezaji pekee raia wa Hispania klabuni Chelsea aliyechaguliwa kuungana na timu yake ya taifa kushiriki michuano hiyo ya kombe la dunia akiwaacha wenzake Marcos Alonso, Cesc Fabregas na Pedro Rodriguez. Lakini nafasi yake kwenye kikosi cha Hispania itakuwa kwenye ushindani akipambana na nyota kadhaa kwenye ulinzi wa kulia. Hana uhakika mkubwa wa kupata nafasi lakini tunaamini akipata nafasi atafanya makubwa.

Argentina
Majeraha ya mlinda mlango nambari moja wa timu hiyo ya taifa, Sergio Romero yanamfanya mlinda mlango nambari mbili wa Chelsea, Willy Caballero kujihakikishia nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo ya taifa ambayo inahitaji ishinde taji hilo huku ikiwa na kumbukumbu mbaya ya kupoteza fainali tatu za mwisho walizoshiriki. Moja ya kombe la dunia mwaka 2014 na mbili za Copa America.

Nigeria
Nyota watatu wa Chelsea wapo kwenye kikosi hiki cha wababe wa Afrika Magharibi, Victor Moses, Ola Aina na Kenneth Omeruo ambaye amekuwa akitolewa kwa mkopo. Victor Moses ambaye ni winga wa Chelsea ana uhakika wa nafasi katika kikosi hicho cha 'Super Eagles' wakati kwa upande wa Ola Aina aliyeitumikia Chelsea kwenye ngazi ya akademi na kupelekwa kwa mkopo kwenye klabu ya Hull city aliyoitumikia msimu uliopita atabaki kama mchezaji wa akiba sambamba na nyota mwenzake wa Chelsea, Kenneth Omeruo.

Denmark
Ni kinda bora klabuni Chelsea na amekuwa na msimu mzuri akiziba vyema pengo la David Luiz kwenye safu ya ulinzi ya Chelsea, kinda Andreas Christensen ameiongoza vyema timu yake hiyo kufudhu kucheza michuano hiyo na amekuwa akitumika kama chaguo la kwanza kwenye safu ya ulinzi na bila shaka ataendelea kushikilia usukani wa ukuta wa timu hiyo.

No comments:
Post a Comment