Kumekuwa na wasiwasi mkubwa kwa klabu ya Chelsea ambapo taarifa kadhaa zinadai mmiliki wa klabu hiyo, Roman Abramovich kutaka kuiuza klabu hiyo huku kusitisha kwake kufatilia kibali kipya cha kuishi nchini Uingereza kukitajwa kama moja ya hatua ya tajiri huyo wa Urusi kutaka kuiuza klabu hiyo.
Hii ni habari mbaya kwa kila shabiki wa Chelsea haswa kutokana na mafanikio aliyoyaleta tajiri huyo tangu alipoinunua Chelsea kutoka kwa mmiliki wa zamani, Ken Bates.
Lakini hilo linatajwa kama nafasi nzuri kwa tajiri na mtoto wa mfalme kutoka nchini Dubai, Hamdan bin Mohammed Al Maktoum maarufu kama Fazza ambaye kuna taarifa zinadai ana mpango wa kuinunua klabu hiyo ya jijini London.
Hamdan Al Maktoum aliwai kusoma nchini Uingereza na amekuwa maarufu sana haswa kutokana na uandikaji wake wa vitabu ambavyo huvipa majina ya Fazza jina ambalo limemfanya kutambulika na kujikuza sana kwenye dunia ya waandishi.
Fazza mwenye miaka 35 anatajwa na vyanzo kadhaa vya habari kuwa yupo tayari kuinunua Chelsea ambayo juzi ilitoa tangazo la kusimamisha mipango yote ya upanuzi wa uwanja wake wa Stamford Bridge huku sababu inayohisiwa ni kutokana na Abramovich kukaribia kuiuza klabu hiyo huku mkataba wake wa kibali cha kuishi nchini Uingereza kikiisha toka mwezi Aprili na sasa anaishi nchini Israel kwenye jiji la Tel Aviv ambapo huko ndiye tajiri zaidi akiwa na utajiri wa paundi bilioni 9.5 wakati Fazza akitajwa kuwa na utajiri unaozidi dola za Marekani milioni 400.
No comments:
Post a Comment