Jumamosi iliyopita ilikuwa ni siku ya muhimu kwa nyota wa zamani wa Chelsea, John Terry ambapo alishindwa kuisaidia klabu aliyomaliza nayo mkataba wa mwaka mmoja, klabu ya Aston Villa kufudhu kucheza ligi kuu Uingereza kwa msimu ujao mara baada ya kupoteza fainali ya mtoano kwenye kugombania kufudhu ligi kuu ambapo ilipoteza kwa goli 1-0 dhidi ya Fulham.
Baada ya mchezo huo zikapita siku kadhaa hatimaye gwiji mwenzake kwenye klabu ya Chelsea na timu ya taifa ya Uingereza, Frank Lampard akatangazwa rasmi kuwa kocha wa klabu ya Derby County ya nchini Uingereza ambayo inashiriki ligi daraja la kwanza nchini humo maarufu kama Championship.
Mara baada ya kutangazwa kuwa kocha mpya wa klabu hiyo, Frank Lampard mwenye miaka 39 alisema tayari ameshafanya mawasiliano na John Terry na kumuuliza kuhusu ugumu na mwenendo wa ligi hiyo yenye timu 24 na akisema anaamini atapata msaada mkubwa kutoka kwa mkongwe mwenzake huyo ambaye kwa sasa ana miaka 37.
Kauli hiyo imetafsiriwa na chombo cha habari cha nchini Uingereza kama kumkaribisha John Terry klabuni hapo.
Lakini kama John Terry atakamilisha kutua Derby County basi itamlazimu kukubali kupunguziwa mshahara aliokuwa analipwa akiwa Aston Villa ambapo alikuwa analipwa paundi 60,000 wakati klabuni Derby County wachezaji wanaolipwa mshahara mkubwa ni nusu ya mshahara huo aliokuwa analipwa mlinzi huyo aliyewai kutamba na Chelsea kwa miaka 22.
No comments:
Post a Comment