Willian Borges aibeba Brazil, na matukio mengine ya kimataifa - Darajani 1905

Willian Borges aibeba Brazil, na matukio mengine ya kimataifa

Share This

Ni siku kadhaa zimesalia kabla ya kuanza kwa michuano yenye thamani kubwa zaidi kwenye tasnia ya mchezo wa soka kama sio duniani, michuano ya kombe la dunia itakayochezwa huko nchini Urusi. Kuelekea kwenye michuano hiyo, kumekuwa na mfululizo wa michezo ya kirafiki ya timu za taifa ambazo nyengine zinajiandaa na michuano hiyo wakati nyengine zikicheza michezo hiyo ya kirafiki kama kujiweka sawa.

Hapa nakuletea michezo iliyochezwa jana usiku iliyowahusisha nyota wa klabu ya Chelsea.

Brazil 2-0 Croatia
Brazil: Nyota wa Chelsea, Willian Borges da Silva alikuwa uwanjani kwa dakika zote 90' za mchezo kuiongoza timu yake hiyo kupata ushindi huo ambao magoli yake yalipatikana kipindi cha pili yakifungwa na Neymar pamoja Firmino.

Hispania 1-1 Switzerland
Hispania: Nahodha msaidizi wa Chelsea, Cesar Azpilicueta alicheza mchezo huo kwa dakika zote za mchezo lakini hapa akitumika kama mlinzi wa kati sambamba na Gerard Pique wa Barcelona.

Mchezo wa usiku wa leo;
Usiku wa leo kutakuwa na mchezo mmoja utakaomhusisha nyota wa Chelsea, Davide Zappacosta ambaye ataiongoza timu yake ya taifa ya Italia kucheza dhidi ya Uholanzi.

No comments:

Post a Comment