Artulo Vidal aifikiria Chelsea - Darajani 1905

Artulo Vidal aifikiria Chelsea

Share This

Chanzo cha Bild kimeripoti taarifa kwamba nyota wa klabu ya Bayern Munich ambaye ni raia wa Chile, Arturo Vidal amechagua kujiunga na klabu mojawapo kati ya Chelsea au Napoli.

Vidal ambaye aliwai kutamba na klabu ya Juventus amekuwa akihusishwa kwa muda mrefu kutakiwa na Chelsea ingawa mara zote usajili huo umekuwa ukionekana kushindikana.

Lakini sasa taarifa hiyo inaweza kuirudisha tena Chelsea ili imsajili nyota huyo.

Bayern Munich hawapo tayari kumuuza lakini mkataba wa nyota huyo umebakiza mwaka mmoja hali inayowaumiza kichwa viongozi wa Bayern Munich ambao wanahofia kama akicheza mpaka mkataba wake ukimalizika maana yake ataondoka bure.

No comments:

Post a Comment