Barcelona yaandaa mpango mpya ili kumnasa Hazard - Darajani 1905

Barcelona yaandaa mpango mpya ili kumnasa Hazard

Share This

Chombo cha habari cha nchini Hispania kimetoa ripoti mpya kuhusu nyota wa Chelsea, Eden Hazard ambaye amekuwa akihusishwa kukaribia kuondoka klabuni hapo.

Chombo hicho cha habari ambacho ni redio kimeripoti kwamba klabu ya Barcelona ipo tayari kumtumia nyota wake Ousmane Dembele ili kumnasa Eden Hazard kutoka Chelsea.

Taarifa hiyo inaeleza klabu hiyo ipo tayari kutoa pesa pamoja na nyota wake huyo raia wa Ufaransa ili imnase Eden Hazard ambaye amebakiza mkataba wa miaka miwili wa kuendelea kuitumikia Chelsea.

Dau la pesa ambalo Barcelona wanataka kulitumia ili kumpata Hazard bado halijatajwa ingawa kunaelezwa biashara hiyo inaweza ikafanyika.

No comments:

Post a Comment