Mambo 3 muhimu ya kuyajua kuhusu jezi mpya za Chelsea kwa msimu wa 2018-2019 - Darajani 1905

Mambo 3 muhimu ya kuyajua kuhusu jezi mpya za Chelsea kwa msimu wa 2018-2019

Share This

Klabu ya Chelsea imezitangaza jezi zake za ugenini itakazozitumia kwa msimu wa 2018-2019 ambapo itatumia jezi zenye rangi ya njano.

Yajue haya kuhusu jezi hizo.
1. Hii sio mara ya kwanza kwa Chelsea kuvaa jezi zenye rangi ya njano. Mara ya kwanza kabisa ilikuwa mwaka 1963.
2. Hii ni mara ya kwanza kwa Chelsea kutumia rangi ya bluu katika soksi zake sambamba na jezi ya rangi ya njano. Mara zote pale inapokuwa na jezi za njano imekuwa ikitumia soksi zenye rangi sawa na jezi zake.
3. Msimu wa 2007-2008 ndo ulikuwa msimu wa kwanza kwa jezi za njano za Chelsea kutumika katika fulana pekee huku ikitumia rangi nyeusi kwenye bukta na soksi.

No comments:

Post a Comment