Leo ni siku ya kumbukumbu ya nyota raia wa Ivory Coast, Didier Drogba ambapo tarehe kama ya leo mwaka 2004 alijiunga rasmi na klabu ya Chelsea akitokea nchini Ufaransa ambapo huko alikuwa akiichezea klabu ya Olympique Marseille.
Usajili wake wa kutua Chelsea ulikamilika kwa dau la paundi milioni 24 na kumfanya kuwa mchezaji wa kwanza kutokea nchini Ivory Coast kuwai kununuliwa kwa dau hilo. Iyo ilikuwa ni mwaka 2004.
Nadhani wengi tunajua makubwa na mazito aliyoyafanya akiwa na klabu ya Chelsea na hata timu yake ya taifa.
Katika kumbukumbu hii nataka tugusie kitu kuhusu maisha yake ambayo mimi mwandishi yananipa funzo kubwa haswa kutokana na kampeni yangu ya "Charity For The Blues" ambayo niliianzisha maalumu kwa kutumia ushabiki wetu katika soka kuleta furaha kwa jamii yetu.
Achana na lile tukio alilolifanya mwaka 2006 akiwa na timu yake ya taifa ambapo alisaidia kusimamisha vita iliyokuwa ikiendelea nchini kwao kwa miaka mitano. Nataka niigusie hii, nyota huyo ana taasisi yake ya ‘Didier Drogba Foundation’ ambayo aliwai kujenga hospitali nchini kwao kwenye jiji la Abidjan akitumia paundi milioni 3 alizolipwa kutokana na udhamini wake na kampuni ya vinywaji vya Pepsi ambapo klabu ya Chelsea pia ikaamua kuungana nae katika kazi zake za kusaidia jamii haswa ya kiafrika.
Kwasasa anatumika kama balozi wa kusisitiza amani na kurudisha amani katika jamii haswa akitumika kutokana na umaarufu wake katika soka. Mpaka sasa taasisi yake imeshafanya mengi katika jamii yake lakini yote yamekuja kutokana na mchezo wa soka.
Hii inanipa imani mimi na blog hii ya Darajani 1905 nikiamini kuna makubwa tunaweza kuyatimiza kwa jamii ili turudishe furaha kwa wale wasiojiweza.
#CharityForTheBlues
No comments:
Post a Comment