Moja kati ya habari zilizokiki toka kwa klabu ya Chelsea ichague kikosi chake cha wachezaji 25 cha kwenda nchini Australia ambapo huko itacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Perth Glory ni juu ya kuachwa kwa nyota wa klabu hiyo, Kurt Zouma.
Tovuti ya habari za michezo ya Goal.com imetoa taarifa kwamba kwanini kocha wa klabu hiyo, Maurizio Sarri asilitaje jina la nyota huyo raia wa Ufaransa.
Inaelezwa sababu kubwa ni kutokana na mlinzi huyo kupata majeraha na hivyo kocha Sarri kuona haina haja ya kumuita nyota huyo huku akiamini ni bora akabaki Uingereza ili afanyiwe matibabu.
Nyota huyo aliyesajiliwa na Chelsea mwaka 2014 akitokea klabu ya St. Etienne ya nchini Ufaransa alitolewa kwa mkopo msimu uliopita kwenye klabu ya Stoke city lakini kabla ya kujiunga na klabu hiyo alisaini miaka sita ya kuichezea Chelsea.
Wachezaji 25 walioitwa ni; Marcin Bulka, Jared Thompson, Bradley Collins, David Luiz, Ethan, Ampadu, Fikayo Tomori, Michael Hector, Tomas Kalas, Marcos Alonso, Emerson, Davide Zappacosta, Ola Aina, Cesc Fabregas, Danny Drinkwater, Tiemoue Bakayoko, Ross Barkley, Mario Pasalic, Jorginho, Kasey Palmer, Pedro, Lucas Piazon, Charly Musonda, Callum Hudson-Odoi, Alvaro Morata na Tammy Abraham
No comments:
Post a Comment