Willian na Barcelona kumekucha - Darajani 1905

Willian na Barcelona kumekucha

Share This

Taarifa zilizopo zinadai nyota wa Chelsea, Willian Borges ambaye kwasasa yupo mapumzikoni ndiye anashawishi kuondoka klabuni Chelsea huku ikielezwa anataka kujiunga na Barcelona.

Kabla ilikuwa ikizaniwa kuondoka kwa kocha Antonio Conte kutamfanya nyota huyo raia wa Brazil abaki klabuni Chelsea lakini pamoja na kocha huyo kuondoka huku Chelsea ikimtangaza Maurizio Sarri kuwa kocha mpya lakini bado hiyo sio sababu ya kumfanya nyota huyo atake kubaki Chelsea.

Tetesi za Willian kutakiwa na Barcelona zilionekana kushamiri pale nyota huyo alipoonyesha uwezo mkubwa katika michezo ya nyumbani na ugenini katika michuano ya klabu bingwa barani Ulaya wakati klabu hizo zilipomenyana mwanzoni mwa mwaka huu na sasa inaelezwa nyota huyo yupo tayari kutimkia nchini Hispania kujiunga na mabingwa hao wa ligi kuu Hispania maarufu kama La Liga.

No comments:

Post a Comment