Kocha wa zamani wa Chelsea, Antonio Conte anatajwa kutaka kufika katika ngazi za kisheria ili kuishtaki klabu ya Chelsea ambayo ilimtimua siku kadhaa toka kocha huyo aanze mazoezi rasmi na kikosi cha nyota ambao hawakushiriki michuano ya Kombe la Dunia ambao kwasasa wapo nchini Australia wakijiandaa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Perth Glory.
Kocha huyo analalamika kwamba kama Chelsea ingetangaza mapema kwamba haimhitaji basi angepata klabu ambayo angeweza kuifundisha na sio kumfukuza kipindi kama hiki ambacho klabu nyingi ambazo zimekuwa zikisaka makocha wapya tayari zimeshawaajiri makocha hao.
Inaaminika kama kocha huyo angetimuliwa mara baada ya kumalizika kwa msimu basi angeweza kuajiriwa na klabu kama Real Madrid ambayo ilikuwa ikihusishwa kumfukuzia kocha huyo muitaliano
Chelsea ilimfukuza kazi kocha huyo siku nne mara baada ya kuanza kusimamia mazoezi na hivyo kumaanisha kocha huyo atalipwa paundi milioni 9 kama fidia ya kumvunjisha mkataba uliosalia mwaka mmoja.
No comments:
Post a Comment