Eden Hazard, Kante, Thibaut Courtois na nyota wengine kulikosa Ngao ya Hisani - Darajani 1905

Eden Hazard, Kante, Thibaut Courtois na nyota wengine kulikosa Ngao ya Hisani

Share This

Nyota saba wa kikosi cha Chelsea ambao ni Eden Hazard, N'Golo Kante, Thibaut Courtois, Michy Batshuayi, Ruben Loftus-Cheek, Gary Cahill, pamoja na Olivier Giroud hawatoweza kushiriki kwenye mchezo wa Ngao ya Hisani dhidi ya Manchester city utakaochezwa tarehe 5-Agosti mwaka huu.

Nyota hao watashindwa kushiriki kwenye mchezo huo kutokana na tarehe zao za kurejea klabuni wakitoka kwenye mapumziko kuwa ni tarehe 5-Agosti na tarehe 6-Agosti kwa nyota wawili waliocheza fainali ya Kombe la Dunia ambao ni N'Golo Kante na Olivier Giroud.

Mchezo huo utaangukia tarehe ambayo nyota hao watakuwa ndo wanarejea klabuni wakitoka kwenye mapumziko hivyo kuwa ni jambo lisilowezekana kurejea na kuingia uwanjani.

No comments:

Post a Comment