Gary Cahill ahofia mabadiliko ya Chelsea, atakiwa na Man utd - Darajani 1905

Gary Cahill ahofia mabadiliko ya Chelsea, atakiwa na Man utd

Share This

Chanzo kimoja cha habari kimeripoti kwamba nahodha wa Chelsea, Gary Cahill anaweza kujiunga na klabu ya Manchester united.

Cahill anahofia kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza mara baada ya Chelsea kukaribia kumnasa mlinzi raia wa Italia anayeichezea klabu ya Juventus, Danielle Rugani mwenye miaka 23.

Cahill ambaye amekuwa nahodha mkuu klabuni Chelsea akichukua majukumu hayo kutoka kwa gwiji John Terry ambaye aliondoka Chelsea mwaka 2017.

Kama Cahill akikamilisha uhamisho wa kujiunga na klabu hiyo, atakuwa mchezaji watatu wa Chelsea kujiunga na Manchester united toka mwaka 2012. Wengine wakiwa ni Juan Mata na Nemanja Matic.

No comments:

Post a Comment