Klabu nyengine ya Italia yatua kwa Alvaro Morata - Darajani 1905

Klabu nyengine ya Italia yatua kwa Alvaro Morata

Share This

Klabu ya Chelsea ilimnasa akitokea klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania kwa dau la paundi milioni 60.  Na toka amefika klabuni Chelsea alianza akiwa na msimu mzuri huku akifanya vyema kwenye majukumu yake ya ufungaji akifunga magoli nane kwenye michezo nane ya mwanzoni lakini baadae alionekana kucheza chini ya kiwango akikosa nafasi nyingi za wazi katika mashambulizi ambayo Chelsea iliyafanya kwa msimu uliomalizika.

Lakini mara baada ya msimu wake mmoja kuutumia klabuni Chelsea huku akishinda nayo taji moja la Kombe la FA lakini kulienea fununu kwamba nyota Alvaro Morata hana furaha ya kubaki klabuni Chelsea.

Klabu ya Juventus ilikuwa ni klabu ya kwanza kutajwa kumfukuzia nyota huyo huku akionekana na moja ya viongozi wa klabu hiyo ingawa baadae alipoulizwa alisema amefika nchini Italia kutokana na kuhudhuria shughuli ya moja wa marafiki zake.

Lakini sasa kuna taarifa mpya zilizosambaa kumhusu mhispania huyo ambapo inaelezwa nyota huyo anatajwa kufukuziwa na klabu ya AC Milan ambao wanaelezwa kuwatuma baadhi ya maboss zake ili kufanya mazungumzo na nyota huyo. Viongozi hao wanatajwa kuweza kutua jijini London ili kukutana na nyota huyo.

Una maoni gani katika hili

No comments:

Post a Comment