Msikie kocha wa Ubelgiji alichokisema kuhusu Hazard kuondoka Chelsea - Darajani 1905

Msikie kocha wa Ubelgiji alichokisema kuhusu Hazard kuondoka Chelsea

Share This

Michuano ya Kombe la Dunia imemalizika huku mabingwa wakiibuka timu ya taifa ya Ufaransa na washindi wa pili wakiwa ni timu ya Croatia lakini timu anayoichezea winga na nyota wa Chelsea, Eden Hazard, timu ya Ubelgiji wakishika nafasi ya tatu.

Lakini kama unavyojua mara kadhaa kocha wa timu ya taifa ya Ubelgiji, Roberto Martinez amekuwa akimsifia nyota huyo ambaye alikuwa nahodha wa kikosi hicho ambacho kimefanikiwa kuibuka washindi watatu wa michuano hiyo mara baada ya kuibamiza timu ya Uingereza.

Ila sasa kuna habari ambazo sio nzuri kwetu mashabiki wa Chelsea, taarifa zinadai kocha huyo ambaye aliwai kuwa kocha wa klabu ya Everton ya nchini Uingereza amemshauri winga huyo kuachana na  klabu ya Chelsea akidai huu ni wakati wa nyota huyo kuachana na klabu hiyo aliyoichezea kwa miaka sita toka aungane nayo mwaka 2012.

Kocha huyo anadai ili Hazard apate mafanikio zaidi na azidi kutambulika kwenye dunia ya soka basi ni lazima aachane na Chelsea.

Hazard amekuwa akihusishwa mara kadhaa kutakiwa na klabu ya Real Madrid ambayo inamsaka nyota atakayeziba pengo la mchezaji Cristiano Ronaldo aliyeachana na klabu hiyo na kujiunga na klabu ya Juventus ya nchini Italia.

No comments:

Post a Comment