Rasmi; Mount akamilisha usajili, aeleza sababu ya kujiunga na Derby County ya Lampard - Darajani 1905

Rasmi; Mount akamilisha usajili, aeleza sababu ya kujiunga na Derby County ya Lampard

Share This

Nyota wa klabu ya Chelsea ambaye ni zao la akademi ya klabu hiyo akiwa na historia ya kushinda tunzo ya mchezaji bora kwenye akademi ya Chelsea, Mason Mount amekamilisha uhamisho wake wa kujiunga kwa mkopo na klabu ya Derby County ya nchini Uingereza.

Mason Mount ambaye msimu uliopita alifanya vizuri akiwa kwa mkopo kwenye klabu ya Vittesse ya nchini Uholanzi ametoa sababu ya kwanini amechagua kujiunga na klabu hiyo ambayo kwasasa inaongozwa na gwiji wa Chelsea, Frank Lampard ambaye ni kocha mkuu wa klabu hiyo.

"Mimi ni kiungo, nacheza nafasi ya kiungo. Kufika kwangu hapa nimekuja kwasababu ya Frank Lampard, nimekuwa nikivutiwa na uwezo wake alipokuwa mchezaji. Nimekuwa nikijifunza mengi kutoka kwake. Nadhani ni sahihi kucheza chini ya nyota wangu."

"Jody (Morris) pia niliwai kufanya nae kazi, nadhani ni uamuzi sahihi kuwa hapa" alisema nyota huyo mwenye miaka 19

Derby County ipo chini ya Frank Lampard huku msaidizi wake akiwa ni Jody Morris ambaye alikuwa kocha wa klabu ya vijana wenye umri chini ya miaka 18 klabuni Chelsea.

No comments:

Post a Comment