Mlinda mlango mwengine wa Chelsea akamilisha usajili wa kuondoka Chelsea - Darajani 1905

Mlinda mlango mwengine wa Chelsea akamilisha usajili wa kuondoka Chelsea

Share This

Mlinda mlango na kinda ambaye chimbuko lake ni akademi ya Chelsea, Jamal Blackman amekamilisha uhamisho wake wa mkopo wa kujiunga na klabu ya Leeds United ya nchini Uingereza.

Blackman ambaye amekuwa akitumika kutolewa kwa mkopo kwenye klabu kadhaa amejiunga na klabu hiyo ambayo ataitumikia kwa mkopo wa msimu mzima.

Unadhani huu ni uamuzi mzuri kwa klabu ya Chelsea? maamuzi haya yamefanywa na bodi ya Chelsea ikiongozwa na mwanamama Marina Glanovskaia ambaye ndiye anasauti ya mwisho katika maswala ya usajili klabuni Chelsea.

Kumbuka siku kadhaa zilizopita mlinda mlango nambari tatu wa Chelsea, Eduardo alisaini mkataba mpya klabuni Chelsea lakini akatolewa kwa mkopo.

Ambapo hiyo inaifanya Chelsea ibakiwe na walinda milango wawili tu (Thibaut Courtois na Willy Caballero) kwanini asingebakizwa Blackman ili awe kipa nambari tatu na aweze kupata nafasi ya kupata uzoefu klabuni Chelsea?

No comments:

Post a Comment