Pamoja na ugeni wake lakini Maurizio Sarri aanza kupatwa na hofu - Darajani 1905

Pamoja na ugeni wake lakini Maurizio Sarri aanza kupatwa na hofu

Share This

Toka ametambulishwa rasmi siku ya tarehe 14-Julai mwaka huu mpaka kufikia hii leo zimepita siku mbili, au sio kwa wale wataalamu wa hesabu mtakuwa mmenisaidia hapo.

Sasa kuna gazeti moja barani Ulaya limeripoti kwamba kocha mpya wa Chelsea, Maurizio Sarri ameanza kupatwa na hofu mara baada ya kuripotiwa taarifa kwamba klabu ya Chelsea inaweza ikampoteza kiungo wake, N'Golo Kante ambaye anafukuziwa na klabu kadhaa ikiwemo klabu za Barcelona na PSG.

Kante ambaye jioni ya jana aliiongoza timu yake ya taifa ya Ufaransa kushinda taji la Kombe la Dunia amekuwa akifukuziwa kwa karibu na klabu ya PSG lakini klabu ya Barcelona inatajwa kuanza kumfukuzia kutokana na kumpoteza kiungo wake mkongwe, Andres Iniesta.

Kante aliwai kuhojiwa kuhusishwa kwake kutakiwa na klabu ya PSG ambapo alisema yupo Chelsea kwa msimu wa pili na anajiona yupo nyumbani.

No comments:

Post a Comment