Chelsea yaandaa fungu nono kumbakisha Hazard - Darajani 1905

Chelsea yaandaa fungu nono kumbakisha Hazard

Share This

Winga na nyota wa Chelsea, Eden Hazard anaweza akasaini mkataba mpya  klabuni Chelsea, mkataba utakaomfanya kuzidi kuwa mchezaji anayelipwa zaidi klabuni Chelsea.

Taarifa zilizopo zinadai Chelsea imeandaa mkataba utakaomfanya winga huyo raia wa Ubelgiji kupokea kitita cha paundi 300,000 kwa wiki, mshahara ambao utamfanya kuzidi kukaa kileleni zaidi.

Kwasasa nyota huyo analipwa paundi 250,000 kwa wiki na ndiye anayeongoza kulipwa mshahara mkubwa lakini kama akisaini mkataba huo mpya utazidi kumfanya kuwa kileleni zaidi.

Mkataba wake wa sasa unamalizika mwaka 2021.

No comments:

Post a Comment