Chelsea yaendeleza ubabe, yaitandika Brighton - Darajani 1905

Chelsea yaendeleza ubabe, yaitandika Brighton

Share This

Klabu ya soka ya wanawake ya Chelsea maarufu kama Chelsea FC Women imefanikiwa kuondoka na ushindi wa magoli 3-2 dhidi ya klabu ya Brighton katika mchezo wa kwanza wa ligi kuu Uingereza (FA WSL) kwa msimu huu wa 2018-2019.

Chelsea iliyokuwa nyumbani, Kingsmeadow ilifanikiwa kupata huo kupitia kwa nyota wake Fran Kirby, Spence na Bethany ambao walikamilisha karamu hiyo na kuifanya klabu hiyo kuanza vyema kampeni yake ya kutetea ubingwa wake huo wa ligi kuu Uingereza.

Chelsea FC Women itaanza pia kampeni yake ya kutetea ubingwa wa Kombe la FA (SSE) ambayo iliibuka mabingwa msimu uliopita lakini pia ikiwa na nafasi ya kushiriki michuano ya klabu bingwa barani Ulaya kwa wanawake msimu huu mara baada ya msimu uliopita kufika hatua ya nusu fainali.

No comments:

Post a Comment