Chelsea yaibaragaza Arsenal, Sarriball yazidi kutamba - Darajani 1905

Chelsea yaibaragaza Arsenal, Sarriball yazidi kutamba

Share This

Chelsea inafanikiwa kuondoka na ushindi mwingine katika mchezo wake wa pili wa ligi kuu Uingereza mara baada ya usiku huu kuitandika Arsenal magoli 3-2.

Kipindi cha kwanza kiliisha kwa matokeo ya 2-2 ambapo Chelsea ndio ilianza kufunga magoli mawili yaliyofungwa na Pedro Rodriguez na Alvaro Morata kabla ya Arsenal kusawazisha magoli yote.

Goli la ushindi lilifungwa na Marcos Alonso aliyefunga goli la tatu katika dakika ya 81 ya mchezo akionganisha pasi murua iliyopigwa na Eden Hazard aliyeingia kama mchezaji wa akiba.

Ushindi huu wa magoli 3-2 unaifanya Chelsea kulelea kileleni mwa msimamo wa ligi kuu Uingereza huku ikiwa na alama 6 lakini ikiwa na faida ya magoli manne.

Uchambuzi;
Nadhani sasa kuna haja ya Ross Barkley akatumika kama mchezaji wa akiba huku Matteo Kovacic akianza pamoja na N'Golo Kante na Jorginho kwenye safu ya kiungo huku Eden Hazard akianza sambamba na Pedro au Willian wakati kule kwa Alvaro Morata nafikiri ingekuwa sawa kama asingepewa nafasi ya uhakika zaidi ya kuanza na badala yake Olivier Giroud atumike kama mshambuliaji chaguo la kwanza. Morata anaonekana kuwa hatari sana pale anapocheza na walinzi ambao wameshachoka.

No comments:

Post a Comment