Ligi kuu Uingereza; Habari muhimu kuelekea Chelsea vs Arsenal - Darajani 1905

Ligi kuu Uingereza; Habari muhimu kuelekea Chelsea vs Arsenal

Share This

Usiku wa leo kunachezeka mchezo wa ligi kuu Uingereza, ukiwa ni mchezo wa pili kwa Chelsea itakayokuwa nyumbani kumenyana dhidi ya Arsenal iliyochini ya kocha Unai Emery.

Kuelekea mchezo huo, hapa nakuletea habari muhimu kuhusu mchezo huo.

Kuhusu mchezo;
Ni mchezo wa wiki ya pili ya msimu wa 2018-2019 wa ligi kuu Uingereza na unawakutanisha makocha wapya kwenye ligi hiyo ya nchini Uingereza. Maurizio Sarri akiiongoza Chelsea huku Unai Emery akiiongoza Arsenal. Utakuwa mchezo wa ushindani lakini Chelsea ikipewa nafasi kubwa kuondoka na ushindi haswa kutokana na morali waliyokuwa nayo kutokana na ushindi iliyoupata kwenye mchezo uliopita wakati ilipoibamiza Huddersfield magoli 0-3,

Tofauti na Arsenal ambayo imepoteza mchezo wake wa kwanza ikiwa nyumbani kwa magoli 1-2 ilipomenyana dhidi ya Manchester city. Lakini pia Chelsea kucheza nyumbani kunaifanya kuzidi kuipa nafasi kubwa kushinda mchezo huo.

Chelsea:
Cesc Fabregas anaweza kuukosa mchezo wa leo kutokana na majeraha aliyokuwa nayo aliyoyapata kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Arsenal hivyo anaweza kurejea mazoezini wiki ijayo.

Tofauti na Fabregas hakuna mchezaji mwengine aliyeripotiwa kuwa na majeraha. Kubwa jengine ni kuhusu Matteo Kovacic ambaye anaweza akapata nafasi ya kuichezea Chelsea mchezo wa kwanza usiku wa leo.

Kikosi cha Chelsea; Kepa Arrizabalaga, Cesar Azpilicueta, David Luiz, Antonio Rudiger, Marcos Alonso, N'Golo Kante, Jorginho, Barkley, Alvaro Morata, Pedro Rodriguez na Willian.

Mwamuzi:
Martin Atkinson amechaguliwa kuwa mwamuzi wa mchezo wa ligi kuu Uingereza kati ya Chelsea dhidi ya Arsenal. Mchezo utakaochezwa jumamosi ya tarehe 18-Agosti.

Mwamuzi huyo amekuwa mwamuzi katika michezo 35 ambayo Chelsea imekuwa ikicheza uwanjani huku katika michezo hiyo, Chelsea imeondoka na ushindi katika michezo 20 na kutoa sare michezo 7 huku ikipoteza michezo 8.

Yani hii inamaanisha katika michezo ambayo mwamuzi huyo amekuwa akishiriki, basi Chelsea ina 57% ya kuondoka na ushindi.

Muda; Saa 7:30 Usiku (Saa 19:30) kwa saa za Afrika Mashariki

No comments:

Post a Comment