Kocha Sarri afanya mkutano kuelekea mchezo wa Chelsea vs Arsenal - Darajani 1905

Kocha Sarri afanya mkutano kuelekea mchezo wa Chelsea vs Arsenal

Share This
Kocha Maurizio Sarri amefanya mkutano na waandishi wa habari hii leo akijibu maswali ya waandishi kabla ya mchezo wa kesho wakati Chelsea itakapokuwa nyumbani ikicheza dhidi ya Arsenal.

Hapa nakuletea baadhi aliyoyazungumza kwenye mkutano huo alioufanya kwenye uwanja wa mazoezi wa Chelsea maarufu kama Cobham Training Centre huko jijini London nchini Uingereza.

Sarri kuhusu Fabregas kucheza mchezo dhidi ya Arsenal: "Natumaini atarejea mazoezini wiki ijayo. Lakini sina uhakika, ni majeraha madogo, lakini yanaweza kumweka nje kwa muda mrefu"

Sarri kuhusu Eden Hazard kuhusishwa kutimkia Real Madrid: "Nimeshaongea nae zaidi ya mara kumi, na hajanambia chochote kuhusu Madrid. Naamini ataendelea kuwa nasi"

Sarri kuhusu kocha wa Arsenal, Unai Emery: "Nafikiri Emery ni kocha bora. Ameshinda Kombe la Europa mara tatu akiwa na Sevilla na bado akashinda ligi kuu akiwa na PSG. Nadhani atafanya makubwa na ana nafasi kubwa kugombania nafasi ya UEFA"

Sarri kuhusu Mateo Kovacic: "Mateo ni mchezaji mzuri, atatusaidia sana lakini sidhani kama ataweza kwa dakika zote 90, nafikiri yupo sawa kucheza kwa dakika 30 za mwishoni"

Lakini pia aliulizwa kuhusu majanga yaliyotokea nchini kwao Italia ambapo kocha huyo alitoa salamu zake za huzuni kuhusu tukio hilo.

No comments:

Post a Comment