Nyota na kinda wa Chelsea, Ola Aina amekamilisha uhamisho wa mkopo wa kujiunga na klabu ya Torino inayoshiriki ligi kuu nchini Italia.
Ola Aina amekamilisha uhamisho wake huo wa pili kwa mkopo ambapo msimu uliopita alitolewa kwa mkopo kwenye klabu ya Hull city inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini Uingereza akiwa sambamba na mlinzi mwenzake kutoka Chelsea, Fikayo Tomori ambaye msimu huu amejiunga na Derby County.
Aina ambaye ni zao la akademi ya Chelsea ni raia wa Nigeria na mara kadhaa amekuwa akipata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha wakubwa cha Chelsea amejiunga na klabu hiyo na kupewa jezi yenye namba 34.
No comments:
Post a Comment