Klabu ya Chelsea inaweza kumpoteza mlinzi wake raia wa Uingereza, Gary Cahill ambaye anatajwa kutokuwa na furaha kuendelea kusalia klabuni hapo.
Kukosa nafasi katika kikosi cha kocha Maurizio Sarri kunatajwa kuwa sababu ya kumfanya mlinzi huyo kuhusishwa kuondoka.
Klabu ya Galatasaray ya nchini Uturuki imekuwa ikitajwa kupeleka maombi kwa mwanamama Marina Glanovskaia ambaye ndiye kiongozi anayeshughulika na maswala ya usajili klabuni Chelsea ili wamsajili nyota huyo ambaye alipokea majukumu ya unahodha kutoka kwa nahodha wa zamani klabuni Chelsea, John Terry mwaka 2017.
Inahisiwa pia, kutafutwa kwa nahodha mpya klabuni Chelsea ambapo wanaohusishwa na Eden Hazard na Cesar Azpilicueta kunamaanisha kufungua milango kwa gwiji huyo kuondoka klabuni hapo.
No comments:
Post a Comment