Klabu ya Chelsea inajiandaa kukataa ofa yeyote itakayotumwa kwa mlinzi wa klabu hiyo raia wa Hispania, Marcos Alonso.
Taarifa zinasema kwamba klabu ya Atletico Madrid ya nchini Hispania inajiandaa kutuma ofa ili kumsajili nyota huyo mwenye miaka 27.
Chelsea ilifanikiwa kumnasa Alonso mwaka 2016 akitokea klabu ya Fiorentina ya nchini Italia.
Nyota huyo ana mkataba na Chelsea unaomalizika mwaka 2021.
No comments:
Post a Comment