Chelsea yapata bahati mwamuzi aliyechaguliwa kuchezesha mchezo dhidi ya Newcastle - Darajani 1905

Chelsea yapata bahati mwamuzi aliyechaguliwa kuchezesha mchezo dhidi ya Newcastle

Share This
Chelsea itasafiri mwisho wa wiki hii kwenda kucheza mchezo wake wa tatu wa ligi kuu Uingereza kwa msimu wa 2018-2019 katika uwanja wa St. James' Park ili kucheza dhidi ya Newcastle siku ya tarehe 26- Agosti mwaka huu.

Kuelekea kwenye mchezo huo, kumefanyika utambulisho rasmi wa mwamuzi atakayetumika kwenye mchezo huo utakaochezwa majira ya saa 18:00 kwa saa za Afrika Mashariki.

Paul Tierney ndiye mwamuzi aliyechaguliwa kuwa mwamuzi mkuu katika mchezo huo.

Uteuzi wa mwamuzi huyo mwenye miaka 37 aliyezaliwa jijini Wigan nchini Uingereza unaonekana kuwa mzuri kwa Chelsea haswa kutokana na rekodi ya mwamuzi huyo pindi anapokuwa mwamuzi kwenye mchezo ambao Newcastle united wanakuwa uwanjani.
Paul Tierney alipokuwa mwamuzi wakati
Newcastle ilipofungwa 3-1 dhidi ya Manchester city kwenye ligi kuu Uingereza
msimu wa 2017-2018

Katika michezo mitano ambayo mwamuzi huyo amekuwa mwamuzi mkuu wakati Newcastle united imekuwa uwanjani basi klabu hiyo imepata ushindi katika mchezo mmoja dhidi ya Barnsley mwaka 2016 huku ikipoteza michezo minne.

Chelsea haijawai kuamuriwa na mwamuzi huyo.

Chelsea itashuka kwenye mchezo huu ikihitaji kuondoka na ushindi ili ijiweke sawa kwenye msimamo wa ligi kuu Uingereza ambapo kama ikifanikiwa kuondoka na ushindi basi itafikisha alama 9.

No comments:

Post a Comment