Abramovich apanga kufanya mabadiliko ya Chelsea - Darajani 1905

Abramovich apanga kufanya mabadiliko ya Chelsea

Share This

Mmiliki wa klabu ya Chelsea, Roman Abramovich anatajwa kuwa na mpango wa kufanya mabadiliko katika nembo ya klabu hiyo ya nchini Uingereza.

Taarifa zinadai kwamba mmiliki huyo anataka kuifanyia mabadiliko nembo ya klabu hiyo uku akilenga kuleta mvuto mpya.

Kama hilo likikamilika basi hii itakuwa mara ya pili chini ya umiliki wake klabuni hapo kuwai kubadilishwa kwa nembo hiyo. Mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2005 ambapo alibadilisha nembo iliyokuwa na herufi CFC pamoja na uwepo na simba na kuileta nembo yenye jina kamili la Chelsea Football Club.

No comments:

Post a Comment