Chama cha soka barani Ulaya, UEFA kupitia kiongozi wake kimetoa taarifa kwamba kimefikia maamuzi ya kuanzisha michuano mipya ya ligi itakayozihusisha klabu za bara hilo.
Michuano hiyo mipya inatajwa kuja na mabadiliko ya kupunguza timu za ligi ya Ulaya (Europa League) kutoka timu 48 zilizopo kwasasa na kufikia timu 32 sawa na michuano ya Klabu bingwa Ulaya (UEFA Champions League). Michuano hiyo itashirikisha timu za klabu na inatajwa kupangwa kuanza msimu wa 2020-2021 uku ikijumuisha klabu 32.
Kama michuano hiyo itaanzishwa basi itafanya michuano ya timu za klabu kushirikisha timu 96 yaani timu 32 kutoka Klabu bingwa Ulaya, timu 32 kutoka Europa League na timu nyengine 32 katika michuano hiyo mipya.
Huu ni mfululizo wa mabadiliko yanayofanywa na chama hicho ambacho mwaka huu kimefungua michuano mipya ya ligi inayoshirikisha timu za taifa 55 ambazo zinazopatikana barani humo maarufu kama UEFA Nations League.
No comments:
Post a Comment