Juventus kupeperusha ndoto za Maurizio Sarri - Darajani 1905

Juventus kupeperusha ndoto za Maurizio Sarri

Share This

Ndoto ya Sarri inaelekeza kufifia. Hilo ndilo unaloweza kulisema kwasasa mara baada ya chanzo cha kuaminikia cha nchini Italia kuripoti habari ambayo kwa kocha wa Chelsea, Maurizio Sarri zinaweza kumfanya akasirishwe nazo.

Chombo hicho maarufu kimeripoti kwamba klabu ya Juventus ipo kwenye mpango wa kumpa mkataba mpya nyota wa klabu hiyo, Danielle Rugani.

Taarifa hizi zinakuja muda mfupi toka wakala wa nyota huyo raia wa Italia kukiri kwamba Chelsea ilikuwa tayari kutoa dau nono ili kumnasa nyota huyo lakini usajili huo ukashindikana kutimia.
kalidou Koulibaly akiwa na klabu ya Napoli

Hii ni habari mbaya kwa Sarri kivipi? inaaminika mara baada ya klabu ya Napoli kukataa kumuuza mlinzi wake nyota klabuni hapo, Kalidou Koulibaly inaaminika kwamba kocha Sarri aliagiza klabu ya Chelsea imfukuzie Rugani ili azidi kuimarisha safu ya ulinzi ambayo kwasasa imewashuhudia nyota wake Antonio Rudiger na David Luiz kutumika kwenye michezo yote minne ya mwanzo.
Danielle Rugani akiwa anaitumikia  timu ya taifa ya Italia

Lakini sasa kwa klabu hiyo kuandaa kumpa mkataba mpya ni kama itafifiisha ndoto za kocha Sarri kumpata nyota huyo ambaye ilikuwa inaaminika kwamba Chelsea ingemfukuzia nyota huyo mwezi Januari kwenye dirisha dogo la usajili au kwenye kubwa la usajili la mwishoni mwa msimu.

No comments:

Post a Comment