Rasmi: Ratiba ya Chelsea dhidi ya Liverpool yawekwa hadharani - Darajani 1905

Rasmi: Ratiba ya Chelsea dhidi ya Liverpool yawekwa hadharani

Share This
Mwezi uliopita, yaani mwezi Agosti kulifanyika upangwaji wa droo ya michuano ya kombe la ligi nchini Uingereza maarufu Kombe la Carabao au unaweza kuyaita Carabao Cup uku Chelsea ilipangiwa kucheza dhidi ya Liverpool kwenye hatua ya raundi ya tatu.

Lakini wakati droo hiyo ikifanyika na michezo hiyo kupangwa lakini haikuwekwa wazi ni siku na tarehe gani ya michezo hiyo ya raundi ya tatu itachezwa. Ukiwemo mchezo wa Chelsea dhidi ya Liverpool ambayo imepangwa kuchezwa kwenye uwanja wa Liverpool maarufu kama Anfield.

Ila leo kumetolewa taarifa kamili ya ratiba ya siku ya michezo hiyo.itachezwa huku Chelsea dhidi ya Liverpool ikipangwa kuchezwa siku ya jumatano ya tarehe 26-Septemba mwaka huu.

Mchezo huu utakuja kabla ya siku tatu wakati Chelsea tena itakapocheza dhidi ya Liverpool katika mchezo wa ligi kuu Uingereza utakaochezwa tarehe 29-Septemba kwenye uwanja wa Stamford Bridge.

No comments:

Post a Comment