Klabu ya soka ya wanawake ya Chelsea maarufu kama Chelsea FC Women, hapo jana ilianza kampeni yake ya kutetea ubingwa wa ligi kuu Uingereza kwa soka la wanawake kwa kucheza mchezo wake wa kwanza wa ligi hiyo, ikicheza dhidi ya Manchester city.
Kipindi cha kwanza cha mchezo huo kilianza uku Karen Carney akiiongoza Chelsea akiwa kama nahodha mkuu kwa mara ya kwanza toka alipotangazwa kuwa nahodha wa klabu hiyo wiki iliyopita. Akichukua mikoba ya aliyekuwa nahodha klabuni hapo, Katie Chapman ambaye amestaafu soka.
Nyota wa klabu hiyo, Fran Kirby alianzia nje kwenye mchezo huo kutokana na kutokupona vizuri majeraha yake aliyoyapata kwenye mchezo wa kugombania tiketi ya kufudhu kwa michuano ya Kombe la Dunia kwa wanawake itakayofanyika mwakani ambapo alikuwa akiichezea timu yake ya taifa ya Uingereza maarufu kama Lioness.
Mchezo ulianza na kipindi cha kwanza kikiisha kwa sare ya kutokufungana. Sare ya 0-0.
Kipindi cha pili, Fran Kirby akapata nafasi ya kupata namba uku pia Erin Cuthbert nae akiingia lakini bahati haikuwa kwa Chelsea ambayo ilitengeneza nafasi nyingi lakini umakini ulikosekana kwenye kumalizia mashambulizi. Hatimaye dakika tisini za mchezo zikakamilika uku ukiisha kwa sare ya 0-0.
Kwa matokeo haya yanamaanisha sasa Chelsea FC Women imeanza ligi hiyo ikiwa na alama moja sambamba na klabu hiyo ya Manchester city.
No comments:
Post a Comment