Chelsea yaanza vibaya ligi kuu - Darajani 1905

Chelsea yaanza vibaya ligi kuu

Share This
Usiku wa jana ulikuwa usiku mbaya kwa klabu ya wanawake ya Chelsea mara baada ya kushindwa kupata matokeo mazuri katika msimu wake wa kugombania ubingwa wake wa michuano ya ligi kuu Uingereza kwa wanawake, FA WSL mara baada ya kutoka suluhu ya 0-0 dhidi ya klabu ya Bristol city.
Klabu hiyo ya Chelsea FC Women ilishuka uwanjani katika mchezo huu ikihitaji alama tatu ili ijiweke sawa katika mbio zake za kutetea ubingwa wake wa ligi kuu ambapo imepata sare ya pili katika mchezo wa pili mfululizo.
Kikosi cha Chelsea kilianza na nyota wote ambapo Fran Kirby, Ramona Bachmann, Ji So-Yun, nahodha Karen Carney pamoja na Millie Bright lakini hiyo haikuwafanya kupata ushindi wake wa kwanza katika michuano hiyo ambayo Chelsea FC Women ndiye bingwa mtetezi.
Mchezo wa kwanza Chelsea ilitoka sare dhidi ya klabu ya wanawake ya Manchester city uku sasa ikitoka sare ya pili na klabu ya Bristol city.
Chelsea inahitaji kupata ushindi katika mchezo unaofata ambapo itakuwa ugenini kumenyana dhidi ya Everton katika mchezo wa ligi kuu.

Mchezo unaofata:
Everton Women vs Chelsea FC Women
Tarehe: 24-Septemba
Michuano: Ligi kuu Uingereza kwa wanawake (FA WSL)

No comments:

Post a Comment