Europa League: Habari muhimu kuelekea mchezo wa Chelsea dhidi ya PAOK - Darajani 1905

Europa League: Habari muhimu kuelekea mchezo wa Chelsea dhidi ya PAOK

Share This

Ni siku nyengine ya Chelsea kushuka uwanjani ili kucheza mchezo wake wa kwanza wa michuano ya ligi ya Ulaya maarufu kama Europa League kwa msimu huu wa 2018-2019.

Klabu hiyo jana iliwasili nchini Ugiriki ambapo huko ndipo itakapoanza kampeni yake ya kutwaa ubingwa wa michuano hiyo ikicheza dhidi ya PAOK katika uwanja wa Stadio Toumbas.

Hapa nakuletea habari muhimu unazopaswa kuzijua kuelekea mchezo huo ambao unaenda kuzikutanisha kwa mara ya kwanza klabu ambazo hazijawai kukutana katika michuano yoyote.

Chelsea:
Vijana wa Maurizio Sarri watakuwa uwanjani hii leo uku ikiwakosa nyota kadhaa ambao ni pamoja na Eden Hazard, Emerson Palmieri, David Luiz na Mateo Kovacic uku Cesc Fabregas akiungana na kikosi kutokana na kuuguza majeruhi kwa muda mrefu.
Kukosekana kwa Eden Hazard, Sarri alisema nyota huyo amebaki nchini Uingereza kutokana na kujihisi kuchoka na anahitaji muda wa kupumzika. Kusoma zaidi, bonyeza hapa

Alichokizungumza kocha Sarri kuhusu mchezo huu: "Ni klabu nzuri na ni klabu bora, nimewatazama katika michezo kama minne iliyopita naona wana ubora. Na kwa kuwa tunataka kushinda mataji basi inatakiwa tuwe na tahadhari dhidi yao kwa kuwa ni moja ya klabu ngumu katika kundi letu"

Kikosi cha Chelsea kinaweza kuwa hivi: Kepa Arrizabalaga, Cesar Azpilicueta, Gary Cahill, Antonio Rudiger, Marcos Alonso, N'Golo Kante, Jorginho Frello, Cesc Fabregas, Willian Borges, Olivier Giroud na Pedro Rodriguez

PAOK
Klabu hii inashika nafasi ya tano katika msimamo wa ligi kuu nchini kwao Ugiriki uku ikiwa nyota ambaye aliwai kucheza katika ligi kuu Uingereza akiwa na klabu ya Arsenal, Akpoum uku mshambuliaji wao Aleksandar Prijovic akirejea akitokea kwenye majeruhi.
Mchezaji wa zamani wa Arsenal, Chuba Akpoum
akiwa na klabu ya PAOK

Rekodi:
Kocha Maurizio Sarri amekuwa na uwiano mzuri wa kushinda michezo ya hatua ya makundi ambapo msimu wa 2015-2016 akiwa na klabu ya Napoli aliiongoza kupata ushindi katika michezo yote sita ya hatua ya makundi katika michuano hii ya Europa League.

Muda: Saa 07:30 Usiku (Saa 19:30) kwa saa za Afrika Mashariki.

No comments:

Post a Comment