Chelsea yaendeleza ufalme, yazidi kuweka rekodi - Darajani 1905

Chelsea yaendeleza ufalme, yazidi kuweka rekodi

Share This

Chelsea inafanikiwa kupata ushindi wake wa kwanza katika michuano ya Ligi ya Ulaya (Europa League) kwa msimu huu wa 2018-2019 ikiwa katika kundi L mara baada ya kupata ushindi wa goli 0-1 dhidi ya PAOK iliyokuwa nyumbani huko nchini Ugiriki.

Shukrani sana kwa Willian Borges ambaye ndiye mfungaji wa bao hilo na la pekee katika mchezo huo akifunga mara baada ya kupokea pasi murua kutoka kwa Ross Barkley na kuifanya Chelsea kuongoza kwa goli moja katika dakika ya saba tu ya mchezo.

Cesc Fabregas alifanikiwa kurejea tena uwanjani kwa mara ya kwanza toka alipocheza mchezo wake wa mwisho dhidi ya Manchester city katika mchezo wa Ngao ya Hisani ambapo Chelsea ilipoteza mchezo huo na toka mchezo huo ulipoisha alikuwa nje akiuguza majeraha aliyoyapata kwenye mchezo wa kirafiki wakati Chelsea ilipomenyana dhidi ya Arsenal. 

Nyota huyo raia wa Hispania alifanikiwa kupata nafasi ya kuingia akichukua nafasi ya Jorginho Frello.

Mchezo ulianza uku kocha akifanya mabadiliko makubwa katika kikosi kilichoanza katika mchezo huo na kikosi kilichoanza katika mchezo uliopita wakati Chelsea ilipomenyana dhidi ya Cardiff city.

Eden Hazard hakuwa katika sehemu ya kikosi katika mchezo huu dhidi ya PAOK uku katika nafasi yake akianzishwa Willian Borges ambaye katika mchezo huu alianza akiwa kama nahodha, Alvaro Morata alifanikiwa kucheza mchezo huu dhidi ya PAOK wakati katika nafasi yake katika mchezo uliopita alicheza Olivier Giroud, Davide Zappacosta na Andreas Christensen nao walifanikiwa kupata nafasi ya kuanza wakati katika nafasi zao katika mchezo uliopita walicheza Cesar Azpilicueta na David Luiz.

Lakini pia Ross Barkley akianza kwenye nafasi ambayo Mateo Kovacic alicheza kwenye mchezo uliopita.

Rekodi:
1. Willian Borges anakuwa nyota wa kwanza raia wa Brazil kuwai kuwa nahodha wa Chelsea katika mchezo wa kiushindani. 2. Kocha Maurizio Sarri anakuwa kocha wa tatu kuwai kushinda michezo saba katika hatua ya makundi ya michuano ya Europa League. Alifanya hivyo katika michezo sita aliyokuwa na Napoli na jana ulikuwa mchezo wake wa saba katika hatua ya makundi. Wengine ni Diego Simeone na Schimdt.
3. Chelsea haijawai kupoteza mchezo wowote ikicheza dhidi ya klabu kutoka Ugiriki. Katika michezo mitano, Chelsea imeshinda michezo 3 na kutoa sare michezo 2.

No comments:

Post a Comment