Sababu ya mashabiki wa Chelsea kutoonekana kwenye mchezo dhidi ya PAOK - Darajani 1905

Sababu ya mashabiki wa Chelsea kutoonekana kwenye mchezo dhidi ya PAOK

Share This
Usiku wa jana Chelsea ilikuwa nchini Ugiriki kucheza mchezo wake wa kwanza wa michuano ya ligi ya Ulaya maarufu kama Europa League dhidi ya PAOK ambapo walifanikiwa kupata ushindi wa goli 0-1 lilofungwa na Willian Borges.

Lakini unajua kwanini uwanjani Toumbas ulipochezeka mchezo huo hakukuonekana shamrashamra za mashabiki wa Chelsea ambao kwa kawaida huwa wanavalia jezi za klabu hiyo pamoja na bendera zikipepea? na badala yale mashabiki walionekana wakiwa na nguo za kawaida uku wakiwa wametulia sana?

Kuna taarifa zinaeleza kwamba serikali ya nchini Ugiriki ilitoa taarifa kwa mashabiki wa Chelsea watakaosafiri na timu kutoka nchini Uingereza mpaka kufika nchini humo wasivae jezi za Chelsea na wawe karibu na klabu itakapofika nchini humo kutokana na matukio kama hayo ya mashabiki wa timu pinzani kuwa wanapigwa.

Lakini mara baada ya jeshi la polisi nchini humo kutoa tahadhari au taarifa hiyo, kukaripotiwa taarifa kwamba mashabiki wawili wa Chelsea walipigwa na kushambuliwa katika jiji unapopatikana uwanja huo ikiwa ni muda mfupi kabla ya mchezo huo kuanza.

Hivyo ripoti hiyo ikazidisha hofu kwa mashabiki wa Chelsea na ndio maana kama ulishuhudia vyema mchezo ule, hakukuwa na mashabiki wa Chelsea waliovalia jezi au kushika bendera za klabu hiyo kutokana na uvunjifu wa amani ambao hutokea kwa mashabiki wa timu pinzani.

Lakini ndio maana pia mwenyekiti wa Chelsea, Bruce Buck alikuwa anasambaza vyakula kwa mashabiki wa Chelsea uwanjani Toumbas ambapo kulikiwa na tahadhari kubwa kwamba wanaweza wakaenda kununua chakula wakapata madhara.

Lakini kuna jambo lilitokea ambalo kuna shabiki mmoja ambaye alizidisha mapenzi, yeye peke yakrendiye alivaa jezi ya Chelsea bila kuogopa.

Mashabiki wa PAOK wamekuwa wakisifika kwa kufanya vurugu na hii sio mara ya kwanza kwao kufanya matukio kama haya. Lakini pia hii sio.mara ya kwanza kwa mashabiki wa Chelsea kuripotiwa kufanyiwa vurugu ambapo kwenye mchezo wa klabu bingwa barani Ulaya msimu uliopita kuliwai kuripotiwa kwamba mashabiki wa Chelsea walifanyiwa fujo na askari kwenye uwanja wa Camp Nou nchini Hispania mara baada ya kumalizika kwa mchezo dhidi ya Barcelona.

No comments:

Post a Comment