Eden Hazard awaongoza walioachwa kikosi cha Chelsea kitakachocheza dhidi ya PAOK - Darajani 1905

Eden Hazard awaongoza walioachwa kikosi cha Chelsea kitakachocheza dhidi ya PAOK

Share This
Klabu ya Chelsea imefanikiwa kusafiri na kutua nchini Ugiriki hii leo ambapo huko imefika ili kucheza mchezo wake wa kwanza wa ligi ya Ulaya yaani Europa League hapo kesho usiku kwa saa za Afrika Mashariki uku Chelsea ikikaribishwa kumenyana na klabu ya PAOK.

Kikosi kilichosafiri kuelekea kwenye mchezo huo kimewajumuisha nyota wote ambao wamekuwa wakihusika kwenye kikosi cha kwanza cha Chelsea kasoro nyota watano ambao ni Eden Hazard, David Luiz, Emerson Palmieri, Mateo Kovacic na Danny Drinkwater.
Hapa nakuletea sababu zilizosababisha nyota hao wasiweze kusafiri kuelekea kwenye michuano hiyo ambayo Chelsea anashiriki akiwa na kumbukumbu nzuri ya kuwa bingwa wa michuano hii mwaka 2013.

Eden Hazard
Nyota huyo anakosekana katika kikosi hichi siku chache toka alipoiongoza Chelsea kupata ushindi wa magoli 4-1 dhidi ya Cardiff city uku mwenyewe akifunga magoli yake matatu kwenye mchezo mmoja (hat-trick) kwa mara ya pili kwenye michuano ya ligi kuu.

Kukosekana kwa nyota huyo kulitolewa ufafanuzi na kocha Maurizio Sarri ambaye alisema "Mara baada ya kurejea akitokea timu ya taifa aliniambia kwamba anajihisi amechoka, na ata mara baada ya mchezo dhidi ya Cardiff alisema anajihisi amechoka. Kwa hiyo niliona ni vyema akabaki Uingereza ili apumzike"

Vipi kukosekana kwa David Luiz na Emerson Palmieri?
Nyota hawa wanakosekana kutokana na mipango ya kocha mwenyewe akitazama na mchezo unaokuja wakati Chelsea itakapokuwa ugenini kumenyana dhidi ya West Ham katika ligi kuu, mchezo ambao huwa ni mgumu sana haswa kutokana na klabu hizo kutokea jiji moja.

Vipi kuhusu Mateo Kovacic?
Nyota huyo anaachwa kwenye safari hii kutokana na kujiweka sawa haswa kutokana na mchezo uliopita dhidi ya Cardiff city kutolewa uwanjani kutokana na kupata majeraha. Hivyo kocha ameamua kumbakisha ili ajiweke sawa zaidi.

Kikosi kamili kilichosafiri.
Makipa: Kepa Arrizabalaga, Willy Caballero na Marcin Bulka
Walinzi: Cesar Azpilicueta, Antonio Rudiger, Gary Cahill, Andreas Christensen, Marcos Alonso, Davide Zappacosta na Ethan Ampadu
Viungo: Jorginho, N'Golo Kante, Ross Barkley, Cesc Fabregas na Ruben Loftus-Cheek
Mawinga: Victor Moses, Callum Hudson-Odoi, Pedro Rodriguez na Willian Borges
Washambuliaji: Alvaro Morata na Olivier Giroud

No comments:

Post a Comment