Rasmi: Ampadu amwaga wino miaka mitano klabuni Chelsea - Darajani 1905

Rasmi: Ampadu amwaga wino miaka mitano klabuni Chelsea

Share This

Nyota kinda wa Chelsea, Ethan Ampadu amefanikiwa kusaini mkataba mpya klabuni Chelsea akiwa kama mchezaji wa kulipwa.

Nyota huyo ambaye siku chache zilizopita alitimiza miaka 18 toka alipozaliwa mwezi Septemba mwaka 2000 amesaini mkataba huo hii leo, mkataba utakaomfanya awe mali ya Chelsea mpaka mwaka 2023.

Ampadu alisajiliwa na Chelsea akitokea klabu ya Exeter city ya nchini kwao Wales mwaka 2017 na toka amefika Chelsea amekuwa akionyesha uwezo mkubwa mpaka kuchaguliwa nyota wa mchezo katika mchezo wa Kombe la FA msimu uliomalizika dhidi ya Afc Bournemouth.

Nyota huyo pia amefanikiwa kuingia kwenye kikosi cha timu yake ya taifa ya Wales ambapo kwenye michezo ya michuano ya Ligi ya kitaifa barani Ulaya maarufu kama UEFA Nations League alifanikiwa kuichezea michezo yote miwili ambayo timu yake imeshiriki mpaka sasa.

No comments:

Post a Comment