FA yamshushia rungu Frank Lampard - Darajani 1905

FA yamshushia rungu Frank Lampard

Share This

Kiungo wa zamani wa Chelsea na timu ya taifa ya Uingereza, Frank Lampard ambaye kwa sasa ni kocha wa klabu ya Derby County amepigwa faini na chama cha soka nchini Uingereza maarufu kama FA baada ya kukubali kosa alilofanya kwenye mechi ya klabu yake dhidi ya Rothertham ambapo klabu yake ilipoteza kwa goli 1-0.

Kocha huyo mwenye miaka 40 alivuka eneo lake la makocha na kumfuata mwamuzi msaidi na kuanza kujibizana nae kosa lililomfanya kuonyeshwa kadi nyekundu.

Frank Lampard amepigwa faini ya paundi 2,000 kutokana na kosa hilo.

Akizungumza na waandishi Lampard alisema "Nimekubali"

Katika maisha yake ya soka akiwa kama mchezaji, Frank Lampard alipewa kadi mbili nyekundu katika michezo 609 uku katika maisha yake ya ukocha imemchukua michezo saba tu kuonyeshwa kadi hiyo nyekundu.

No comments:

Post a Comment