Chelsea yaitandika Cardiff, yazidi kuweka rekodi - Darajani 1905

Chelsea yaitandika Cardiff, yazidi kuweka rekodi

Share This
Hatimaye Chelsea imefanikiwa kupata ushindi wake wa tano mfululizo katika michuano ya ligi kuu Uingereza ikiibamiza klabu ya Cardiff city jumla ya magoli 4-1.

Mchezo ulianza uku Chelsea ikiruhusu kufungwa goli la mapema mnamo dakika ya 16' kabla ya Eden Hazard kusawazisha mnamo dakika ya 37' akipewa pasi ya mwisho kutoka kwa Olivier Giroud na kufanya mchezo kuwa sare ya 1-1.

Wakati mchezo ukielekea mapumziko, Eden Hazard akafanikiwa kufunga goli la pili likifungwa dakika ya 44' akipokea tena pasi kutoka kwa Olivier Giroud ambaye kwenye mchezo wa leo alipata nafasi kwa mara ya kwanza kucheza kwa dakika zote tisini za mchezo. Goli hilo liliifanya Chelsea kwenda mapumziko ikiwa kifua mbele kwa magoli 2-1.

Kipindi cha pili kilianza uku Chelsea ikiendelea kuumiliki mchezo kwa kiasi kikubwa mpaka kufikia dakika ya 80 ambapo Eden Hazard alifanikiwa kufungwa goli la tatu kwa mkwaju wa penati na kuifanya Chelsea kuwa mbele kwa magoli 3-1 kabla ya Willian Borges kufunga goli la nne na la mwisho katika mchezo huo.

Uchambuzi:
Nategemea kuuona umoja wa Olivier Giroud na Eden Hazard ukiendelea kufanya makubwa sana haswa kutokana na ushirikiano wao kuonekana kuwa mkubwa zaidi. Kwa kiasi kikubwa ushindi wa leo umesababishwa na umahili wao wote wawili.

Rekodi:
1. Magoli matatu ya Eden Hazard katika mchezo wa leo dhidi ya Cardiff city yanamfanya kutimiza magoli 94 toka aliposajiliwa mwaka 2012 na kuingia kwenye nafasi ya tisa katika orodha ya wafungaji bora wa muda wote klabuni Chelsea. Frank Lampard ndiye magoli mengi akishika nafasi ya kwanza akiwa na magoli 211.
2. Kocha Maurizio Sarri anakuwa kocha wa nne kuwai kushinda michezo mitano katika msimu wake wa kwanza katika michuano ya ligi kuu Uingereza. Wengine ni pamoja na Carlo Ancelloti, Craig Shakespeare na Pep Guardiola.
3. Pedro Rodriguez anafanikiwa kuichezea Chelsea mchezo wa 100 katika michuano ya ligi kuu Uingereza.
4. Magoli matatu ya Eden Hazard katika mchezo yanamfanya kuwa mchezaji wa nne klabuni Chelsea kuwai kufunga magoli matatu (hat-trick) zaidi ya mara moja. Wengine waliowai kufanya hivyo ni Didier Drogba, Frank Lampard na Jimmy Floyd Hasselbaink.

No comments:

Post a Comment