Rasmi; Kikosi cha Chelsea dhidi ya Cardiff, pamoja na uchambuzi - Darajani 1905

Rasmi; Kikosi cha Chelsea dhidi ya Cardiff, pamoja na uchambuzi

Share This

Chelsea inashuka uwanjani jioni ya leo, ili kucheza mchezo wake wa tano wa ligi kuu Uingereza dhidi ya Cardiff city. Hapa nakuletea kikosi cha Chelsea na uchambuzi kuhusu mchezo huo utakaochezwa kwenye uwanja wa Stamford Bridge. Mchezo unachezwa saa 5:00 Jioni (Saa 17:00) kwa saa za Afrika Mashariki.

Kikosi cha Chelsea:

Kocha Maurizio Sarri amefanya mabadiliko katika nafasi ya ushambuliaji akimuanzisha Pedro Rodriguez ambaye kwenye mchezo uliopita alianza kama mchezaji wa akiba dhidi ya Bournemoutn. Ambapo aliingia na kuchukua nafasi ya Willian Borges.

Lakini pia kocha ameamua kumuanzisha Olivier Giroud ambapo huu ni mchezo wa kwanza kwa mshambuliaji huyo kuanza katika kikosi cha kocha Sarri katika msimu huu wa ligi kuu Uingereza. Alvaro Morata amekuwa akitumika kama chaguo la kwanza lakini katika mchezo wa leo ataanzia benchi. Nyota huyo amefunga goli moja katika michezo minne ya ligi kuu msimu huu.

Uchambuzi:
Nafikiri ni sahihi kwa maamuzi ambayo kocha ameamua kuyafanya. Olivier Giroud atakuwa na kujiamini kwa hali ya juu haswa kutokana na kufanikiwa kufunga katika mchezo uliopita wakati alipoitumikia timu yake ya taifa hivyo kumweka katika hali nzuri ya kujiamini. Lakini pia Giroud alihusika vyema katika ushindi wa mchezo uliopita ambapo aliingia kama mchezaji wa akiba na kutoa pasi ya mwisho. Hivyo kunamfanya kujiamini sana na anataka kupambania nafasi kwenye kikosi cha Chelsea. Naamini kutaka kwake kupambania nafasi kutamfanya kucheza kwa umakini na  kuwa msaada mkubwa kwa timu.

Rekodi:
Pedro Rodriguez anaenda kuichezea Chelsea mchezo wa 100 wa ligi kuu Uingereza toka alipojiunga na klabu hiyo.

No comments:

Post a Comment