Ni kwa mara nyengine na siku nyengine imefika kwa michuano ya ligi kuu Uingereza kutimua vumbi mara baada ya kusimama kwa muda kupisha michezo ya kitaifa iliyo kwenye ratiba ya FIFA.
Chelsea inashuka uwanjani jioni ya leo ili kucheza mchezo wake wa tano wa ligi kuu Uingereza ikiwa nyumbani Stamford Bridge kucheza dhidi ya Cardiff city.
Hapa nakuletea habari muhimu unazopaswa kuzijua kuelekea kwenye mchezo huo ambao kama Chelsea ikifanikiwa kupata ushindi basi itafanikiwa kutimiza alama 15 katika michezo mitano ya ligi kuu.
Chelsea:
Chelsea itamkosa Ruben Loftus-Cheek ambaye anakosekana kutokana na majeraha aliyoyapata akiwa na timu yake ya taifa ya Uingereza uku ikielezwa atakaa nje kwa wiki mbili. Lakini pia inaelezwa Cesc Fabregas ataukosa mchezo wa leo kutokana na kutokuwa sawa kimwili kutokana na kuwa majeruhi. Davide Zappacosta na Emerson Palmieri nao kuna wasiwasi wakakosekana.

Cardiff:
Gunnarsson na Mendez-Laing nao wanatajwa kukosekana kwenye mchezo wa leo kwa upande wa Cardiff city kutokana na majeraha pamoja na kutokuwa sawa kwa ajili ya mchezo.
Gunnarsson na Mendez-Laing nao wanatajwa kukosekana kwenye mchezo wa leo kwa upande wa Cardiff city kutokana na majeraha pamoja na kutokuwa sawa kwa ajili ya mchezo.
Mwamuzi:
Jonathan Moss ndiye mwamuzi katika mchezo huu wa leo. Ukiachana na mchezo wa Ngao ya Hisani mwaka huu wakati Chelsea ilipomenyana dhidi ya Manchester city, katika michezo tisa ambayo mwamuzi huyo amekuwa kati wakati Chelsea ilipocheza, Chelsea imefanikiwa kupata ushindi katika michezo yote.

Rekodi:
Klabu hizi mbili hazina historia kubwa katika kukutana, lakini Chelsea ina rekodi nzuri pindi inapokutana na klabu hii. Katika msimu wa mwisho kukutana ilikuwa msimu wa 2013-2014 na Chelsea ikafanikiwa kupata ushindi katika michezo yote miwili, mchezo wa kwanza uliochezwa Stamford Bridge ukiisha kwa Chelsea kupata ushindi wa mabao 4-1 wakati mchezo wa pili Chelsea ilikuwa ugenini ambapo huko napo ilifanikiwa kupata ushindi wa mabao 1-2. Mara ya mwisho kwa Chelsea kupoteza dhidi ya Cardiff city kwenye ligi ilikuwa mwaka 1981 ambapo Chelsea ilipoteza kwenye michuano ya Ligi daraja la pili, ikipoteza kwa goli 0-1.
Muda: Saa 05:00 Jioni (Saa 17:00) kwa Saa za Afrika Mashariki
No comments:
Post a Comment