Sarri aelezea uwezekano wa John Terry kurejea Chelsea - Darajani 1905

Sarri aelezea uwezekano wa John Terry kurejea Chelsea

Share This
Gwiji wa soka raia wa Uingereza, John Terry amekuwa akihusishwa kwa karibu kutakiwa na klabu kadhaa ikiwemo klabu ya Aston Villa aliyomalizana nayo mkataba mwezi Juni mwaka huu mara baada ya kuitumikia kwa mwaka mmoja.

Klabu ya Spartak Moscow ya nchini Urusi nayo ilikuwa ikitajwa kwa karibu kumfukuzia nyota huyo mpaka akafanyiwa nayo vipimo ili ajiunge nayo kabla ya usajili huo kushindikana kutokana na John Terry kusema alipofanya mazungumzo na familia yake hawakuridhia gwiji huyo mwenye miaka 37 kujiunga na klabu hiyo ambayo ilikuwa tayari kumpa mkataba wa miaka miwili na mshahara wa paundi milioni 1.8 baada ya makato kwa mwaka.

Lakini kushindikana kwa usajili kumezusha taarifa mpya juu ya nyota huyo kudaiwa anaweza akarejea klabuni Chelsea lakini kwasasa akiwa kama mtu wa benchi la ufundi.
Na jambo hilo limetolewa ufafanuzi na kocha Maurizio Sarri ambapo alipohojiwa alikiri kwamba aliwai kumshawishi nyota huyo aliyeichezea Chelsea kwa miaka 22 ajiunge na Chelsea lakini kwa wakati huo Terry alisema anatamani kuendelea kucheza kwanza.

"Mara ya mwisho nilipozungumza nae alisema bado anataka kuendelea kucheza. Japo Chelsea ni kama nyumbani kwake. Lakini kama akiwa tayari nipo tayari kuwa nae" alisema kocha Maurizio Sarri.

Mara kadhaa gwiji huyo amekuwa akitembelea uwanja wa mazoezi wa Chelsea na msimu uliopita aliwai kuhudhuria mazoezi ya klabu hiyo pindi iliokuwa chini ya kocha Antonio Conte.

No comments:

Post a Comment