Derby County yapoteza uku Lampard akitolewa uwanjani - Darajani 1905

Derby County yapoteza uku Lampard akitolewa uwanjani

Share This

Jana ilikuwa siku nyengine kwa kocha wa klabu ya Derby County, Frank Lampard kuiongoza timu yake katika mchezo wa ligi daraja la kwanza nchini Uingereza maarufu kama Championships ambapo alikuwa ugenini kucheza dhidi ya Rothertham united ambapo mchezo huo uliisha kwa Derby County kupoteza kwa goli 1-0.

Derby County ilicheza pungufu katika mchezo huo kutokana na mchezaji wao kupewa kadi nyekundu na kutolewa nje na kusababisha Rotherham kupata penati na kufanikiwa kufunga goli pekee katika mchezo huo.

Lakini kubwa lilitokea ilipofika dakika ya 77' ambapo kocha wa Derby County ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa Chelsea, Frank Lampard alipoonyeshwa kadi nyekundu kwa kumlalamikia mwamuzi wa pembeni kuhusu mwamuzi wa kati kukataa kutoa penati kwa klabu yake.

Lampard alionekana kutoridhika na maamuzi yaliyotolewa na mwamuzi wa kati na kumsababisha kulalamika.

Malalamiko yake yakamfanya mwamuzi wa kati akimuonyesha kadi nyekundu na Lampard kutakiwa kuondoka kwenye sehemu ya benchi la ufundi.

Huenda ni nadra sana kushuhudia makocha wakionyeshwa kadi kama ilivyotokea kwa Lampard lakini hii ni kanuni mpya iliyopitishwa katika michuano hiyo kwa waamuzi kuruhusiwa kutoa kadi kwa makocha wanaoonekana kuvunja sheria. Gwini huyo atasuniri adhabu kutoka kwa chama cha soka kama ni adhabu gani atapewa kama kufungiwa michezo au kulipa faini au yote mamwili.

No comments:

Post a Comment