ANTONIO CONTE KUMFUKUZA HAZARD - Darajani 1905

ANTONIO CONTE KUMFUKUZA HAZARD

Share This
Wachezaji wa Chelsea wanahofia huenda mshambuliaji wa timu hiyo Eden Hazard ataondoka endapo Kocha wa timu hiyo Antonio Conte ataendelea kukifundisha kikosi hicho.


Eden Hazard (27) amebakisha miaka miwili tu kwenye mkataba wake na timu hiyo huku mabingwa hao watetezi kombe la ligi kuu ya England (EPL) wakiwa kwenye mikakati  ya kumuongeza mkataba mpya.
Chelsea wamejiandaa kumlipa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji kiasi cha Euro 300000 kwa wiki ili nyota huyo aweze kubaki  klabuni hapo lakini bado mshambuliaji huyo bado hajakubali kuweka mkataba mpya.

Chanzo cha habari cha Daily Telegraphy kinasema Wachezaji wa Chelsea wana wasiwasi na uhusiano kati ya Hazard na Conte na kusema mfumo wa kocha huyo umeshusha kiwango cha mshambuliaji huyo.

Mapema mwezi huu, Hazard aliongea hadharani kuwa hana furaha na mbinu za kocha huyo baada ya kichapo cha 1-0 dhidi ya Manchester City ambapo mchezaji huyo alipocheza kama namba 9 (false no, 9) na kupelekea Conte kuchukizwa na mchezaji huyo.

No comments:

Post a Comment