Kocha Antonio Conte leo amefanya mkutano kuelekea mchezo dhidi ya Leicester katika hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la FA hapo siku ya jumapili. Mkutano huo ambao huufanya kwa kawaida kila baada ya siku moja ama mbili au muda mfupi kabla ya Chelsea kushuka uwanjani ameongea mambo mengi, akijibu maswali yaliyoulizwa na waandishi wa habari, na hapa nakuletea baadhi ya maswali hayo na majibu aliyoyatoa.
Alipoulizwa juu nyota wa Chelsea, Gary Cahill pamoja na Alvaro Morata kuachwa na timu zao za taifa ambazo zitacheza michezo ya kirafiki mwishoni mwa mwezi huu alisema "Jukumu langu ni kuhakikisha wachezaji wanakuwa kwenye ubora wao, kuhusu kuchaguliwa kwenye timu za taifa nadhani hilo swali linawahusu makocha wao wa timu za taifa. Kuhusu kuchaguliwa hilo ni pendekezo la makocha wao"
Alipoulizwa ni nini anakitazama kuelekea mchezo w kombe la Fa dhidi ya Leicester city, kocha huyo alisema "Kiukweli inatakiwa tupambane ili kufika hatua nyengine ya inayofata ya kombe la FA lakini pia tupambane ili kuingia kwenye klabu nne za juu katika ligi kuu"
Alipoulizwa ni mlinda mlango gani atamtumia katika mchezo huo alisema, "Kati ya Caballero au Courtois wote wana nafasi ya kucheza kwenye mchezo huo maana wote ni wazuri.
Alipoulizwa juu ya nini anakiwaza mara baada ya Chelsea kutolewa kwenye michuano ya klabu bingwa Ulaya dhidi ya barcelona, kocha huyo alisema "Halikuwa jambo zuri kwetu kuondoshwa klabu bingwa, lakini haya ndiyo maisha na katika hili inatakiwa tuwe na kujiamini na kuendelea tukiwa na nguvu kabisa" alisema kocha huyo
Hayo ni baadhi ya aliyoyaongea kwenye mkutano wa hivi leo akiiandaa timu kusafiri tena kwenda kumenyana dhidi ya Leicester huko kwenye uwanja wa King Power.
MKUTANO WA ANTONIO CONTE, KUELEKEA MCHEZO WA KOMBE LA FA
Share This
Tags
# Chelsea FC
# Chelsea Habari
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Habari
Labels:
Chelsea FC,
Chelsea Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment