Real Madrid YAIFATA TENA CHELSEA, LAKINI SIO KWA HAZARD - Darajani 1905

Real Madrid YAIFATA TENA CHELSEA, LAKINI SIO KWA HAZARD

Share This
Klabu ya Real Madrid imekuwa ikitajwa kumfukuzia nyota wa Chelsea, Eden Hazard kwa muda mrefu uku ikitajwa kuandaa madau tofauti ili kuishawishi Chelsea imuuze nyota huyo ili akaungane na klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu nchini Hispania. Lakini mpaka sasa zinatajwa tetesi tu juu ya nyota huyo kujiunga na klabu hiyo huku ikielezwa kama Chelsea ikishindwa kufudhu kucheza michuano ya klabu bingwa barani Ulaya msimu ujao, basi nyota huyo ataondoka, lakini sasa klabu hiyo inatajwa kumfukuzia nyota mwengine wa Chelsea tofauti na Eden Hazard.

Marcos Alonso Mendoza ndiye anatajwa kwa sasa kutakiwa na klabu hiyo ili aungane nayo kwa mara nyengine mara baada ya hapo mwanzo kuichezea na kuonekana kutokuwa na maisha mazuri klabuni hapo.

Klabu ya Real madrid inatajwa kuhusishwa na nyota huyo raia wa Hispania, nyota ambaye anaonekana kuaminika zaidi na kocha wa Chelsea, Antonio Conte ambaye amekuwa akimtumia zaidi nyota huyo mwenye sifa kubwa ya kupiga mipira ya adhabu (faulo).

No comments:

Post a Comment